Kupoteza simu yako kunaweza kuwa tukio lenye msongo wa
mawazo hasa ukiwaza kuhusu gharama ya kifaa na taarifa muhimu zilizopo
ndani yake habari njema ni kwamba kuna njia nyingi rahisi za haraka za kufuatilia
na kuipata simu yako iliyopotea au kuibiwa . fuata mwongozo huu hatua
kwa hatua ili kuokoa muda na kuongeza nafasi ya kuipata simu yako.
· Tumia icloud find my iphone kwa watumiaji wa ios
Kwa watumiaji wa iphone ,Apple ina huduma ya find my iphone inayosaidia kufuatilia simu yako.
Ingia kwenye akaunti yako ya icloud kupitia
icloud.com au fungua app ya find my iphone kwenye kifaa kingine cha Apple.
Chagua simu yako kutoka kwenye orodha ya vifaa vinavyohusiana na akaunti yako.
Ramani itaonyesha eneo la simu yako ikiwa
imewasha location services.
SSSOMA PIA:Mambo Sita Yasiyopaswa Kufanywa Wakati Wa Ujauzito
Tumia google find my device kwa simu ya android
Huduma ya find my device ya google ni suluhisho bora kwa watumiaji wa Android hivi ndivyo unaweza kutumia :
Tembelea tovuti ya find my phone au pakua app ya find my phone kwenye kifaa kingine .
Ingia kwa kutumia akaunti ya google uliyokuwa unatumia katika simu yako iliyopotea.
Ukishaingia utaona eneo la simu yako kwenye
ramani ikiwa iko mtandaoni.
SSSOMA PIA:Mabilionea wadogo zaidi duniani mwaka 2025
Chaguo la usalama
·
Play sound:simu italia hata ikiwa kwenye silent
mode
·
Secure Device:weka ujumbe kwenye skrini ya simu
ili anayepata aone na aweze kuwasiliana na wewe
·
Erase Device:futa data zako zote ikiwa huna
matumaini ya kuipata simu.
Tumia program maalumu za kufutia simu
Kabla ya kupoteza simu hakikisha
umesakinisha program za kufuatilia kama:
·
Prey Anti theft:inakusaidia kufuatilia simu yako
kufunga kwa mbali n ahata kupiga picha za mazingira.
·
Cerberus:hutoa udhibiti kamili wa simu hata kama
imezimwa au imebadilishwa laini.
·
Tumia namba ya IMEI kufuatilia simu yako
Namba ya IMEI(international mobile equipment identinty ) ni
kitambulisho cha kipekee cha simu yako.
JINSI YA KUIPATA IMEI YAKO
·
Piga *#06# kabla ya simu yako kupotea
·
Angalia kwenye sanduku la simu au risiti ya
ununuzi.
HATUA YA KUFUATILIA IMEI
·
Toa taarifa kwa polisi ukitumia namba ya IMEI
·
Wasiliana na mtoa huduma wako wa simu kama
Vodacom,Airtel,halotel au yas. Watakusaidia kufuatilia simu au kuzuia
isitumike.
SSSOMA PIA:Wajue wadukuzi wenye nguvu zaidi waliotikisa Dunia kupitia intaneti
WASALIANA NA HUDUMA ZA MTOA MITANDAO.
Ikiwa hatua zote za kufuatilia zimeshindikana wasiliana na
kampuni yako ya mtandao wa simu.
·
Zuia laini yako mara moja ili isiendelee
kutumika vibaya.
·
Wanaweza kusaidia kufuatilia simu yako ikiwa
bado inatumia mitandao wao.
VIDOKEZO VYA KUJILINDA KWA BAADAYE
·
Weka huduma ya find my Device au find my
iphoneikkiwa imewashwa kila wakati
·
Hakikisha unatumia nywira imara au fingerprint
lock kwenye simu yako.
·
Hifadhi nakala za data zako mara kwa mara kwa
kutumia google drive au I cloud.
·
Andika na hifadhi namba yako ya IMEI mahala
salama.
SSSOMA PIA:Programu muhimu kuwa nazo katika kompyuta yako
Simu yako ni kifaa cha thamani kinachobeba
taarifa muhimu hivyo ni vyema kuchukua hatua mara moja ikiwa ikiwa imepotea kwa
kufuata hatua zilizoelezwa hapa unaweza kuokoa simu yako au angalau kulinda
taarifa zako binafsi.
Je umewahi kufuatilia simu iliyoibiwqa au
kupotea shiriki uzoefu wako kwenye sehemu ya maoni hapo chini.